Tuesday, 29 December 2015

Asalaam alaykum.Somo letu la leo ULUL AMR ni nani.waislamu wamegawanyika makundi mawili kuhusu maana ya "ulul amr"yaliyo tumika katika aya ya 59 ya surat nisai.wako wasemao kuwa maana ya maneno haya ni"watawala kutoka miongoni mwenu"yaani watawala wa kiislamu;na hii ndio tafsiri ifuatwayo na waislamu walio wengi yaani(masuni).wako wengine wasemao kuwa,maana ya maneno hayo ni "makhalifa(au maimamu maasumiin(watakatifu)walio teuliwa na allah kushika mahali pa mtukufu(s.a.w.w)baada ya yeye mtume kuondoka hii ndio tafsiri ifuatwayo na mashia ithna-ashariyah.allah anasema katika kitabu chake kitukufu"enyi mlio amini mtiini allah na mtiini rasuli(wake muhammad)na wale waliopewa mamlaka kutoka miongoni mwenu(qur'ani 4:59):amirul muminiin ally bin abi talib(as)anasema yeyote yule amwasiye allah astiiwe.mfano tumchukulie kiongozi mmoja aliyekuwa khalifa wa waislamu yazidi bin muawiyyah yeye alikataa kabisa kumwamini mtukufu mtume (s.a.w.w).alionyesha wazi wazi imani yake katika shairi lake lisemalo:bani hashimu mtume (s.a.w.w)na ahlul-bayt wake walivumbua mbinu kujipatia milki.kwa hakika hakukuwepo na habari zozote zitokazo kwa mwenyezimungu wala ufunuo wowote.ikumbukwe kuwa huyu yazid ndo yule aliyefasiri ile aya kwamba ole wao wenye kuswali watajuta mnaona kwamba mtume (s.a.w.w)wamewaletea majuto basi msimfuate na alikuwa akiwavisha mbwa na ngedere mavazi ya viongozi wa kidini pia alikuwa mcheza kamari mnywa pombe na hakuwa na heshima kwa mwanamke yeyote na hata mahramu wake kama vile mama,shangazi,mama mdogo na mabinti zake hawa wote walikuwa sawa na wanawake wengine mbele yake.je?mtu kama huyu anafaa kutiiwa na tukisoma (Qur'ani 76:24) wala msimtii miongoni mwao mwenye dhambi.

No comments:

Post a Comment