Assalam Alaykum ndugu zetu wafuatiliaji wa ukurasa huu,leo tutawaletea makala ya maisha ya bibi Fatwima A.s ,bint ya Mtume s.a.w.w.Tukianzia ktk suala la IBADA:Ibada aliyokuwa akiifanya bibi huyu ilikuwa ikiendana nakufanana na Ibada ya Mtume S.a.w.w na vilevile Ibada ya Imam Ally A.s,ilikuwa nyumba ya utume ndio mihrab yakuabudiwa M'Mungu mmoja mwenye nguvu,alivyokuwa ktk Nyumba ya baba yake Dini yake ilikuwa ni Ibada na kujinyenyekeza ktk ibada ya Allah,navilevile ktk Nyumba ya mumewe nayo ni nyumba ambayo Allah alishusha aya ya kuwatakasa watu wa Nyumba ya Mtume s.a.w.w,Bibi huyu alikuwa akiutumia muda wake mwingi ktk kumuabudu M,Mungu Mtukufu,imenukuliwa kutoka kwa Imam Hassan A.S amesema "Nimemuona Mama yangu Fatwima A.S ktk mehrabu yake Usiku akiwa anarukuu na kusujudu mpaka Asubuhi nanimemsikia akiwaombea waumini na akiwataja majina,na akizidisha kuwaombea Dua nawala sikumsikia akijiombea yeye mwenyewe,nikamuuliza ewe Mama yangu mbona sijakusikia ukijiombea mwenyewe?akanijibu ewe mwanangu Jirani kwanza kisha nyumbani"tunachotakiwa kijifunza kwa leo ni umuhimu wa wake zetu kuwa ni Nuru ya Ibada ktk majumba yetu,nakufuata mwenendo wa Bibi huyu ktk kuwajali wasiokuwa sisi kwanza kuliko nafsi zetu.inshaallah itaendelea.
No comments:
Post a Comment