Saturday, 3 October 2015

KUSIMAMA KIDETE KWAJILI YA MWENYEZI MUNGU.

Kusimama kidete kwajili ya Mwenyezi Mungu, kunapelekea Jihadi na Mapinduzi ya Kiroho, ndo maana tunaona hakuna jambo gumu kwa Mwanadamu, kama kufanya jambo kwajili ya kupata ukaribu na Muuumba wake,kusimama kidete na kufanya mambo kwajili ya ukaribu na Muumba,kunamfanya Mwanaadamu apande daraja la juu mno ktk ukaribu wake na Muumba wa Ulimwengu na vilivyomo ndani yake,kufanya kazi yoyote ile kwajili ya Mwenyezi Mungu Maana yake ni kufanya Kazi ktk Njia yake,na hili huthibitika kwa Vitendo si kwa Maneno ya Mtu,Tukiona hatuliwezi hilo, sababu itakuwa ni kuruhusu kwetu kuzitii Nafsi zetu na kufuata Matakwa ya Shetani,na ni miongoni mwa Jambo linalofanya Mambo mengi kuishia Njiani, kwahiyo tujitahidi kupambana na Nafsi zetu ili tuupate ukaribu na Muumba ambao ndio Jihadi na Mapinduzi ya kweli.

No comments:

Post a Comment