Friday, 25 December 2015
je?aliyeweka msingi wa jengo lake kwa kumcha mwenyezimungu,mungu na radhi yake ni bora au aliyeweka msingi wa jengo juu ya ukingo wa shimo linalomomonyoka,na likamomonyoka likaanguka pamoja naye katika katika moto wa jahannam?na mwenyezimungu hawaongozi watu madhalimu(9:109)quruan. Takwa ni dhana ya kiislamu ya kuwa na hali ya kujitawala au kujizuia.Neno hili limetumika mara 251 ndani ya quruan ama kama nomino au kitenzi.Neno takwa asili yake ni neno la kiarabu "wa-qa-ya" ambalo maana yake ni ulinzi au msaada.Ni muhimu kutambua kwamba takwa sio kutekeleza mambo ya faradhi ya kidini tu kama vile kuswali na kufunga saumu.Ni kuhusu kuishi maisha ya uchamungu pia kuishi maisha ya kujitenga na maisha ya kinyama na uovu bali kuishi maisha ya uadilifu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment