Tuesday, 22 December 2015
Jumanne, 22 Disemba 2015 18:56
Algeria kuzidisha usimamizi wa uchapishaji Qur'ani

Wizara ya Biashara ya Algeria imetoa amri ya kuzidishwa usimamizi katika uchapishaji wa nakala za Kitabu kitakatifu cha Mwenyezi, Qur'ani, nchini humo.
Shirika la Kimataifa la Habari za Quran (IQNA) limeripoti kwamba, Wizara ya Biashara ya Algeria imetoa agizo hilo baada ya kusambazwa nakala za Qur'ani zilizopotoshwa ambazo baadhi zimepotoshwa katika mpangilio wa sura zake na nyingine sura zake hazikukamilika au zimechapishwa nusu.
Agizo hilo limetolewa kwa Kituo cha Usimamizi wa Viwango cha Idara Biashara ya mkoa wa Muaskar huko kaskazini magharibi mwa Algeria. Kituo hicho kimetakiwa kusimamia na kudhibiti uchapishaji na uuzaji wa nakala za Qur'ani Tukufu.
Tayari maafisa wa mkoa huo wameanza mikakati ya kusimamia uchapishaji wa vitabu vya kidini hususan nakala za Qur'ani Tukufu.
Makosa hayo ya chapa ya nakala za Qur'ani Tukufu yanashuhudiwa zaidi katika nakala zilizochapishwa na taasisi za watu binafsi na kusambazwa masokoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment