Saturday, 13 February 2016

Magufuli: Sitaingilia mzozo Zanziba

MzozoImage copyrightAFP
Image captionRais Magufuli ameshauri wasiokubaliana na hali waende mahakamani
Rais wa Tanzania John Magufuli amesema hataingilia mzozo wa kisiasa ambao unaendelea visiwani Zanzibar kuhusu uchaguzi.
Akiongea na Wazee wa Dar es Salaam, katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja katika vyombo vya habari, Dkt Magufuli amesema hakusudii kamwe kuingilia mzozo huo.
“Kuhusu Zanzibar, kama tume za uchaguzi nyingi duniani, haiwezi kuingiliwa na Rais yeyote ndiyo maana tume za uchaguzi huwa huru,” amesema Dkt Magufuli.
“Napenda kuheshimu sheria. Hiyo ZEC ina uhuru wa kuamua mambo yake lakini kama kuna tafsiri mbaya, waende mahakamani, mahakama ziko pale halafu unamwambia Magufuli ingilia.
Jukumu langu kama amiri jeshi mkuu ni kuhakikisha amani ya Zanzibar inaimarika, yeyote atakaeleta fyokofyko ajue vyombo vya usalama vipo."
Chama cha Wananchi (CUF) mwezi uliopita kilikuwa kimetoa wito kwa kiongozi huyo wa jamhuri ya muungano kuingilia kati.
Mzozo visiwani humo unatokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 20 Oktoba mwaka jana.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza kwamba uchaguzi utarudiwa 20 Machi, hatua iliyopigwa na viongozi wa CUF ambao wamesema watasusia.

Tuesday, 2 February 2016

Basi linalotumia umeme wa jua lazinduliwa Uganda

o
Image captionBasi linalotumia umeme wa jua
Basi linalotumia umeme wa nguvu za jua ambalo limedaiwa na watengezaji wake nchini Uganda kuwa la kwanza barani Afrika limeendeshwa hadharani.
Basi hilo la kielektroniki aina ya Kayoola linalomilikiwa na kampuni ya Kiira Motors lilionyeshwa katika uwanja wa Uganda mjini Kampala.
Mojawapo ya betri zake zinaweza kuwekwa chaji na vibamba vya umeme wa jua katika paa la nyumba ambavyo huongeza kasi ya gari hilo hadi kilomita 80 kwa saa.
Watengezaji wake sasa wanalenga kuwavutia wateja wataolitengeza basi hilo ili kuvutia soko kubwa la magari duniani.
Mkurugenzi mkuu wa Kiira Motors Paul Isaac Musasizi ameiambia BBC kwamba amefurahishwa na jaribio la gari hilo lilipoendeshwa.
Raia wamefurahishwa na wazo kwamba Uganda ina uwezo wa kutengeza mfano kama huu na bw. Musasizi anasema kwamba angependelea kulisaidia taifa hilo kushindana na kampuni nyengine za magari katika eneo hili.
Pia anatumai kwamba hatua hiyo itabuni ajira zifikiazo 7000 kufikia mwaka 2018.Hatahivyo mradi huo hauwezi kuanza bila ya usaidizi wa kampuni zinazotengeza vifaa vya magari.
Image captionBasi linalotumia umeme wa jua
Lengo ni kwamba kufikia 2039,kampuni hiyo itakuwa na uwezo wa kutengeza vifaa vya magari na kuviunganisha nchini Uganda bila kutegemea kampuni nyengine .
Basi hilo lenye viti 35 linalenga kufanya kazi katika miji midogo badala ya mji mkuu kutokana na masharti ya umbali linakoweza kusafiri.
Iwapo mabasi hayo yatazalishwa kwa wingi,kila basi litagharimu kiasi cha dola 58,000 ambacho bw,Musaizi anasema ni bei nzuri katika soko lenye ushindani mkubwa.
Kampuni ya Kiira Motors ilianzishwa kutokana na mradi uliofanyika katika chuo kikuu cha Makerere,ambacho ni mmoja wa mmiliki wa hisa katika kampuni hiyo na pia kimenufaika na ufadhili kutoka kwa hazina ya fedha ya serikali

Ndege ya Iran yapiga picha manowari ya Marekani


Picha
Image captionPicha zilizotolewa na shirika la Irin zinaonyesha manowari ya kuchukulia ndege za kivita
Ndege ya Iran isiyokuwa na rubani ilipaa juu ya manowari ya kutumiwa na ndege za kivita za Marekani na kupiga picha wakati wa mazoezi Ghuba ya Uajemi, shirika la habari la serikali ya Iran limetangaza.
Picha zinazodaiwa kuonyesha manowari ya Marekani ambayo jina lake halikutajwa, imeonyeshwa kwenye runinga na shirika hilo.
Kamanda wa jeshi la wanamaji la Iran amesifu operesheni hiyo kwa kukaribia sana manowari hiyo “na kupata picha za ufasaha kuhusu majeshi ya taifa la kigeni”.
Marekani imesema ndege isiyo na rubani ya Iran ilipaa juu ya moja ya manowari zake, lakini haikusema iwapo kisa hicho ndicho kilichoangaziwa na Iran.
Ndege hiyo haikutoa hatari yoyote kwa USS Harry S Truman, lakini hatua hiyo “haikuwa ya kawaida na haikuwa ya kitaalamu”, shirika la habari la Reuters limemnukuu msemaji wa jeshi la wanamaji la Marekani.
Image copyrightIRIB
Bi Nicole Schwegman amesema kisa hicho kilitokea tarehe 12 Januari, ambayo ndiyo siku Iran iliwazuilia kwa muda mabaharia 10 wa Marekani waliokuwa wameingia maeneo ya bahari ya Iran kimakosa.
Ripoti ya shitika la habari la Iran, Irinn, haukusema ni lini ndege hiyo ilipiga picha hizo ila tu ilitaja kwamba ilikuwa siku ya tatu ya mazoezi ya jeshi la wanamaji.
Shirika la habari la AP linasema hii inaonyesha huenda kisa hicho kilitokea Ijumaa, kwani jeshi la wanamaji la Iran lilianza mazoezi mapema wiki hii.
IranImage copyrightISNA
Image captionNyambizi ya Iran pia inadaiwa kushiriki operesheni hiyo
Nyambizi ya Iran pia ilishiriki katika operesheni hiyo ya kufuatilia shughuli za maadui, shirika la habari la Iran lilisema.
Mkuu wa majeshi ya wanamaji ya Iran Habibollah Sayyari, ameambia runinga ya taifa kwamba hiyo ni ishara ya “ujasiri, uzoefu na uwezo wa kisayansi wa wataalamu wetu wa ndege zisizo na marubani”.
Iran iliondolewa vikwazo ilivyowekewa kutokana na mpango wake wa nyuklia mapema mwezi huu, na kuimarisha uhusiano wake na nchi za Magharibi.
Lakini siku chache baadaye, Marekani iliweka vikwazo kuhusiana na mradi wa makombora ya masafa marefu wa Iran.
Iran ilisema vikwazo hivyo, vinavyoathiri idara 11 na watu binafsi wanaohusika na mpango huo ambao hawataruhusiwa kutumia mfumo wa benki wa Marekani,“havina msingi wowote kisheria na kimaadili”.

Je unaelewa jinsi uchaguzi wa Marekani unavyoendeshwa ?

Image copyrightna
Image captionMwongozo wa kumteua muaniaji urais nchini Marekani
Mwongozo wa kumteua muaniaji urais nchini MarekaniMuhtasari:
Kabla ya Wamarekani kuamua nani wanayemtaka awe rais ajaye, wao kwanza huteua nani atakayewania kiti hicho.
Mchakato huo hungo'oa nanga kwa mchujo wa kamati za wajumbe ambapo wananchi hupata fursa ya kumchagua muaniaji kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha Democratic au kile cha Republican.
Huu hapa ni mwongozo wa mchakato wa kuteua wagombea.
Je mchakato wa kuteua wagombea huwa vipi ?
Image copyrightGetty
Image captionMwongozo wa kumteua muaniaji urais nchini Marekani
Kura za mchujo na mfululizo wa uchaguzi wa kamati za wabunge hufanyika katika kila jimbo na wilaya nje ya nchi ambayo huamua nani atapeperusha bendera ya kila chama.
Mshindi wa mchujo huo anawakusanya wajumbe - hawa ni wanachama wenye nguvu ya kupiga kura kumchagua mgombea katika mikutano ya chama.
Katika makongamano hayo ndipo mgombea wa urais wa kila chama huchaguliwa.
Nini tofauti kati ya kongamano la Chama na mchujo wa mashinani ?
Kongamano la chama kinahusisha wanachama wanaokusanyika katika shule, nyumba za watu binafsi na majengo ya umma kujadili wagombea sera zao na mapendekezo yao
na mara nyingi wao hupiga kura waziwazi kwa kuonyesha mikono.
Hata hivyo katika mchujo wa mashinani wajumbe wa chama cha kisiasa huketi wakajadili sera na mapendekezo ya wagombea na huchagua mgombea wao kwa kupiga kura kwa siri wakitumia sanduku la kura.
Kura za mchujo wa mashinani huandaliwa na serikali ilihali kongamano la chama huandaliwa na watu binafsi vigogo wa chama, wanachama kwa jumla.
Kuna aina mbalimbali za mchujo na sheria mbalimbali:• Mchujo wa wazi -"Open":
Image copyrightGetty
Image captionMjadala wa kuwania tikiti ya Republican ulifanyika katika jimbo la Iowa
Mchujo huu ni wazi kwa kila mtu mwenye kadi ya kupigia kura bila kujali msimamo wa chama.
Hii inamaanisha kuwa japo mtu anaweza kuwa mwanachama wa Republican anaweza kushiriki katika kura za Demcrats.
Kinyume chake pia ni sawa na halali.
• " Mchujo Nusu wazi: - "Semi" :
Hapa wajumbe wanaoruhusiwa kushiriki katika mchujo na upigaji kura sharti wawe ni wanachama waliosajiliwa rasmi katika chama kinachoendesha uchaguzi huo wa mchujo.
Kwa Mfano wanachama wa chama cha Democrat pekee ndio wanaoruhusiwa kushiriki katika mchujo huo wa kumchagua muaniaji tikiti ya urais kwa chama cha Democratic.
Hata hivyo kwa wale wapiga kura ''Huru/Binafsi''ambao hawaegemei upande wowote ima ni Democrat ama Republican wanaweza kushiriki katika mchujo huu.
Jimbo la New Hampshire huwa linaendesha mchujo nusu .
• Mchujo Uliofungwa - "Closed" :
Hapa wajumbe wa chama waliojiandikisha kikamilifu ndio wanaoruhusiwa kupiga kura katika majimbo waliojiandikisha pekee.
Kila mjumbe anaipigia chama chake kura kumchagua muaniaji tikiti wa chama hicho.
Kura za mchujo zinatofautiana katika kila jimbo.
Katika majimbo mengine,wajumbe wa chama cha Democratic huruhusiwa kukiri wazi wazi kuwa wanampendelea mgombea mmoja dhidi ya mwengine.
Hata hivyo katika chama cha Republican mambo huwa ni ya siri.
Image copyrightGetty
Image captionMgombea urais wa Republican Ted Cruz ametumia muda mwingi katika kampeni Iowa
Wajumbe ni nani?
Michujo na kamati za wajunbe hazina uwezo wa kumchagua moja kwa moja mgombea urais.
Hiyo kirasmi na shughuli na jukumu la wajumbe katika mikutano ya vyama .
Wajumbe ni wanachama wa vyama mbalimbali, hivyo wanauwezo wa kumpigia kura muaniaji kiti cha urais kuambatana na matakwa ya wanachama walioshiriki katika mchujo.
Wakati mwengine inawezekana kwamba mgombea hakuweza kupata wajumbe wa kutosha kushinda uteuzi wa chama hicho,na ikifikia hapo basi makubaliano mahsusi kati ya wagombea ndio huamua yupi kati ya washindani wakuu anayechaguliwa kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu.
Mapatanisho na mazungumzo kati ya mawakala wa wagombea wakuu na hata wakati mwengine raundi ya pili na hata ya tatu ya kura miongoni mwa wajumbe wa chama huishia kwa mgombea mmoja.
Si aghalabu wakati mwengine kumpata muaniaji mkuu hata kwenye kura za mchujo hususan pale anapoibuka maarufu mgombea mmoja dhidi ya wenzake mapema katika mchakato huo wa uteuzi.
Hilo likitokea wagombea wenza hujiondoa mapema na kutumia muda wao mwingi kuwapatanisha wafuasi hasidi kwa manufaa ya chama kabla ya uchaguzi mkuu.
Kwa nini Iowa na New Hampshire hupiga kura wa kwanza ?
Hakuna sababu hasa -
Mwaka huu 2016 Kamati za Wajumbe maalum katika jimbo la Iowa watamchagua muaniji kiti cha urais katika chama chao tarehe 1 Februari.
New Hampshire kwa upande waowatashiriki wajibu huo wao wa kikatiba tarehe 9 Februari.
Wahakiki wanadai nchi majimbo hayo mawili hayastahili ushawishi walionayo kwa sababu matokeo hayo si wakilishi kwa idadi kubwa ya wamarekani.
Kwa mfano, Iowa na New Hampshire ni majimbo madogo mno na yanawakilisha haswa maeneo nje ya mijini ambapo idadi ya wazungu ni asilimia 94% ikilinganishwa na asilimia 77 % ya idadi ya wazungu kwa mujibu wa takwimu ya taifa ya.
Image copyrightGetty
Image captionMgombeaji wa tikiti ya Republican Donald Trump ameimarika sana katika kura za maoni
Hata hivyo majimbo hayo mawili yanajipigia debe yakisema kuwa asilimia kubwa ya wapiga kura wao ni wasomi katika maswala ya siasa na wanauweza na tajriba ya kuwawajibisha wagombea mbali na kuhoji sera zao na mashiko yao
Je mgombeaji akiibuka mshindi katika majimbo ya Iowa au New Hampshire huwa ndiye atakaye pigiwa upatu kuwa muaniaji mteule wa chama ?
Si Kweli -
Sio daima kuwa muaniaji kiti cha urais wa chama anayeibuka mshindi katika kongamano la wajumbe katika jimbo la Iowa , ndiye atakayeibuka kuwa muaniaji mteule wa chama.
Hata hivyo muaniaji mteule huko Iowa huibuka na ari ya kuendelea kuwashawishi wajumbe katika majimbo mengine na mara nyingi huwa wanashawishika.
kwa kweli Iowa husaidia kuimarisha ama hata kuvunja ndoto za wawaniaji wengi wa tikiti cha urais katika vyama vyao.
Image copyrightGetty
Image captionLicha ya kutamba kwenye mijadala mgombeaji wa tikiti ya Democratic Martin O'Malley ameshindwa kusisimua wapiga kura
Wahakiki wanasema kuwa kwa sababu New Hampshire ndio uchaguzi wa pili na mara nyingi hupewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari mshindi huko New Hampshire bila shaka anapata muamko mzaidi wa kujibidiisha na kuamini kuwa anaweza kuibuka mshindi wa chama chake.
Vilevile anayeshinda New Hampshire huwa anaendelea kuvutia hisia za wamarekani wengi haswa wale ambao hawakuwa wameamua watamchagua nani wakati wa awali wa kinyang'anyiro hicho cha uteuzi.
Mwandishi wa BBC Katty Kay anasema: "wagombea wanaoibuka na ushindi katika majimbo ya Iowa na New Hampshire huwa wanajenga hisia ya kasi na kwa hiyo huendeleza kasi kampeni yao bila shaka wakiangaziwa zaidi na vyombo vya habari kuliko ilvyokuwa kabla ya ushindi huo.
"Ukishinda Iowa bila shaka utakuwa kwote kwenye televisheni.
''Kisha kuna fedha na Ufadhili- mgombea anapotwaa majimbo hayo mapema, huwa anafungua milango ya ufadhili kutoka kwa wahisani ambao awali walikuwa hawajui wamdhamini nani.''
''Ni ukweli usiopingika kuwa watu wanampenda mshindi ''kila mmoja wetui anapenda mafanikio''.
Image copyrightGetty
Image captionLicha ya kuongoza katika kura za maoni bi Hilary Clinton alishindwa mwaka wa 2008 na rais Barack Obama
Jumanne kuu ni nini?
Jumanne kuu ni siku ambayo majimbo mengi huandaa michujo au kamati za wajumbe kwa wakati mmoja.
Mwezi Februari 2008, majimbo 24 yalishiriki katika "Super-Duper Tuesday ", Katika mwaka 2012 ni majimbo 10 pekee yalioshiriki katika jumanne kuu.
Mwaka huu, Jumanne kuu imeratibiwa kuwa tarehe 1 Machi.
Majimbo 16 yataandaa mchujo na chaguzi katika majimbo 13 ya Marekani.
Kutaadaliwa uchaguzi katika himaya za Marekani .
Image copyrightGetty
Image captionSeneta Bernie Sanders ni mshindani wa karibu zaidi wa bi Hillary Clinton katika kinyang'anyiro cha tikiti ya chama cha Democratic
Nini hufanyika baadaye?
Kamati za wajumbe na michujo itaendelea mpaka majira ya joto, na kisha uteuzi wa waniaji kiti cha urais wa vyama utaidhinishwa rasmi katika mkutano ya kitaifa ya vyama inayoratibiwa kufanyika mwezi wa Julai.
Majimbo yote ya Marekani yatatuma idadi mbalimbali ya wajumbe kuwawakilisha kulingana na ukubwa na rekodi yake ya upigaji kura .
Mgombea lazima ashinde kwa wingi wa kura za wajumbe.
Mshindi sharti apate uungwaji mkono na nusu ya wajumbe na zaidi ili kupata uteuzi wa chama hicho.
Muaniaji kiti cha urais kwa tikiti ya Republican anahitaji kura 1236 za wajumbe iliatangazwe mshindi.
Wakati huohuo muaniaji tikiti ya chama cha Democratic anastahili kutia kibindoni kura 2383 iliajihakikishie kupeperusha bendera ya chama chake katika uchaguzi mkuu ujao.

Serikali yaipongeza Africa Muslim Agency


Yawashukuru wafadhili toka nchi za Kiarabu
Aboud Jumbe ataka amana itunzwe
Na Mwandishi Wetu, Moshi
Serikali imesema kwamba inathamini sana huduma za elimu, afya na ustawi wa jamii zinazotolewa na mashirika ya kidini. 
Aidha Serikali imetoa shukurani kwa wahisani wa miradi hiyo na kusisitiza kwamba Serikali inathamini sana juhudi za mashirika ya dini kwa mchango wake katika kuboresha huduma za jamii na kutoa misaada ya kibinaadamu. 
Hayo yapo katika salamu za Serikali za hivi karibuni katika hafla rasmi ya ufunguzi wa ‘Markaz Al Hudaa’ mjini Moshi ambayo ni taasisi rasmi ya huduma za Elimu, afya na 
ustawi wa jamii. Taasisi hiyo inamilikiwa na Shirika lenye Makao yake makuu Kuwait. 
Akiwasilisha salamu hizo za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Prof. Philemon Sarungi; Afrisa Elimu Bw. Majili aliwataka wasimamizi wa Taasisi hiyo wafikishe salamu na shukrani za dhati za Mkuu wa Mkoa na Serikali kwa ujumla kwa Shirika la Africa Muslim Agency na kwa wahisani wote wanaochangia huduma hizo. 
Kituo hicho cha Al-Hudaa kipo kata ya Kaloleni katika manispaa ya Moshi na kinajumuisha Al-hudaa Secondary School, Al-hudaa Daru-aytama; Eh-Ahsa Health Centre na Darul-Muuminat Vocatinal Centre. 
Taasisi zote hizo zishaanza kufanya kazi ambapo nyumba ya yatima inalea watoto 72, wakati Chuo cha ufundi kimesajili wanawake 25 ambao hujifunza ushonaji, misingi ya uhasibu, hisabati. lugha ya kiingereza na Maarifa ya Uislamu. Shule ya Sekondari itakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita. 
Mzee Aboud Jumbe, Rais Mstaafu wa Zanzibar ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika sherehe hizo aliwaomba watakaonufaika na huduma hizo wazienzi na kwamba hiyo ni amana toka kwa Mola wao. 
Miongoni mwa wageni waliohudhuria sherehe hizo ni Sheikh Muhammad Al-Khamis toka Kuwait; Sheikh Twariq Al-Muhsin na Mar’wa Algamzi kutoka Emarati. 
Wao ni miongoni mwa Waislamu ambao swadaka zao husaidia kuendesha huduma hizo. Akielezea msimamo wa Shirika lake, Mkurugenzi wa Africa Muslim Agency Ofisi ya Dammam Sheikh Muhammad Al-Khamis alisema kuwa Waislamu wenye azma ya kutumia kile walichoruzukiwa kwa njia ya Allah wameamua kutoa huduma mbalimbali ili Waislamu na jamii kwa ujumla ifaidike kwazo. 
Africa Muslim Agency ina Ofisi kuu mjini Dar es Salaam ikiongozwa na Sheikh Shakir; wakati ile ya Kanda ya Kaskazini (Moshi) inaongozwa na Sheikh Majid.

BIBI MARYAM(a.s) Imran was a good man.his wife was called hanna.Hanna made a promise to Allah(s.w.t)that she would give her baby to serve allah.she asked allah to keep her baby safe from shaytan (satan)when her baby was born ,she called maryam.hanna kept her promise and took baby maryam to the place of worship in Jerusalem. Here bibi maryam was looked after by prophet zakariyya (a.s)who was her uncle.One day when bibi maryam was young lady, an angel came to her room and told her that she was to have a baby whose name would be issa son of maryam.The angel told her that her baby would be a prophet of allah.abd would speak even when an infant. Bibi maryam asked the anfel how she could have a baby without a husband. The angel told her that allah could do anything he wished.After prophet isa was born bibi maryam was worried as ti how she.would tell the people of the town about him.she was ordered by allah to keep silent and let the baby talk. When the people asked her about the baby,she pointed to him arms.Baby ( a.s)said:"I am a servant of allah ,he has given me the book(injili)and made me a prophet"qur'an-surah maryam 19:30.