Tuesday, 22 December 2015

Nimaskitiko Makubwa kwa Matukio Yanayoendelea Leo Duniani Ya Umwagaji Wa Damu Za Watu Wasio Na Hatia.

matano, 23 Disemba 2015 06:28 Waislamu wa Kenya wazuia kuuliwa abiria wenzao wa Kikristo na wanamgambo wa al Shabab  Abiria wa Kiislamu waliiokuwa wakisafiri kwa basi na wenzao wa Kikristo huko Kenya wamezuia kuuliwa wenzao katika shambulio la wanamgambo wa al Shabab. Abiria Waislamu waliokuwa ndani ya basi huko Kenya wamekataa kutii amri ya wanamgambo walioshambulia basi hilo ili kuwatambua abiria wa dini ya Kikristo waliokuwa wakisafiri pamoja na Waislamu hao. Shambulio hilo lilijiri Jumatatu wiki hii katika kaunti ya Mandera kaskazini mashariki mwa Kenya, wakati watu waliokuwa na silaha wanaosadikiwa kuwa na uhusiano na kundi la al Shabab la Somalia walipolifyatulia risasi basi hilo lililokuwa na abiria 60 na kuua watu wawili. Abdi Mohamud Abdi abiria Muislamu aliyekuwa miongoni mwa watu waliokuwamo ndani ya basi hilo amesema kuwa, wanamgambo kumi waliiingia ndani ya basi hiyo na kuwataka abiria wa Kiislamu kujitenga na wale wa Kikristo, hata hivyo abiria Waislamu walikataa kutii amri ya wanamgambo hao. Baadhi ya Waislamu ndani ya basi hilo walitoa hijabu zao na kuwapatia wale wasio Waislamu ili kuwasaidia kuficha utambulisho wao wakati basi liliposimama. Itakumbukwa kuwa, mwaka jana wanamgambo wa al Shabab waliokuwa na silaha waliwaua raia wasio Waislamu karibu 30 waliokuwa wakisafari kwa basi katika eneo hilo hilo.

No comments:

Post a Comment