Dkt Ali Mohamed Shein wa Chama cha Mapinduzi CCM amewataka wafuasi wa chama hicho kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio, baada ya Maalim Seif Sharif Hamad wa Chama cha Wananchi CUF kuitisha mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kusema chama chake hakipo tayari kuona uchaguzi unarudiwa. Akihutubia mkutano maalumu wa CCM wa maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika katika Viwanja vya Maisara, Dkt Shein amewataka wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio pindi Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC itakapotangaza tarehe. Kwa upande wake Chama cha Wananchi CUF kimelaumu njama zinazofanywa na baadhi ya watu za kutaka kusababisha machafuko visiwani Zanzibar kwa kushikilia kurudiwa uchaguzi visiwani humo. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea wa urais wa tiketi ya CUF katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015, amesema kuwa, hakuna mashiko yoyote ya kisheria yanayoweza kuhalalisha hatua ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ya kutangaza kufutwa uchaguzi huo na kusema kuwa, uchaguzi wa Oktoba 25 ni halali. Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliingia katika mgogoro wa kisiasa miezi miwili iliyopita baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi kwa kile alichokiita ukiukwaji wa sheria na utaratibu wakati wa zoezi la upigaji kura. Hatua hiyo ilichukuliwa katika hali ambayo matokeo yote ya uchaguzi wa majimbo 54 ya Baraza la Wawakilishi yalikuwa yameshatangazwa pamoja na karibu theluthi mbili ya kura za Urais
Monday, 25 January 2016
Sisitizo la hatua za umoja dhidi ya njama za kuibua mifarakano nchini Iraq

Katika mwendelezo wa hatua za umoja wa wananchi wa Iraq, Waislamu wa Shia na Suni wa mji wa al-Miqdadiyah, katika jimbo la Diyala, hivi karibuni walisali Swala moja ya Ijumaa kwa pamoja
Zaid al-Azawi, gavana wa mji wa al-Miqdadiyah amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, Waislamu hao wa Kisuni na Kishia walisali Swala ya pamoja katika Msikiti wa Laa Ilaha Illallaah uliopo katika mji mdogo wa Ashur. Azawi amesisitiza kuwa, katika swala hiyo ya umoja walishiriki pia maulama wa Kisuni na Kishia, wasomi na shakhsia wa makabila kadhaa ya mji huo. Ameongeza kuwa, Swala hiyo ilisaliwa kwa lengo la kudumisha umoja wa kidini na kitaifa katika kukabiliana na mirengo inayozusha tofauti, na kadhalika kuimarisha umoja wa wakazi wa al-Miqdadiyah wenyewe katika kukabiliana na changamoto ambazo zililikumba eneo hilo siku chache zilizopita.
Kamanda wa polisi wa jimbo la Diyala, Jasim al-Sa'adi, amesisitiza kuwa, kusaliwa Swala hiyo ya umoja, kunaonesha umoja na ushirikiano wa wakazi wa eneo hilo katika kupambana na njama za kutaka kuibua tofauti na fitina baina yao.
Naye Ra'ad al-Mas, mwakilishi wa jimbo la Diyala serikalini amesema kuwa, hivi sasa jimbo hilo hususan mji wa al-Miqdadiyah, lina usalama na amani . Inafaa kuashiria hapa kwamba, wiki iliyopita, mji wa al-Miqdadiyah, ulishuhudia mashambulizi ya kigaidi. Wakati huo huo mwakilishi wa Ayatullah Sistani, marjaa wa kidini nchini Iraq amewataka viongozi wa kisiasa na pande tofauti za nchi hiyo kuweka kando tofauti zao ili kukomesha mpasuko wa ndani nchini humo. Ahmad al-Swafi, amesema kuwa, hii leo Iraq inakabiliwa na matatizo na changamoto kubwa, zaidi likiwa ni jinamizi la kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh. Sanjari na kuwataka wanasiasa wa Iraq kufanya juhudi za kuimarisha usalama na amani nchini, amewataka wanasiasa kuyaunganisha makundi tofauti ya wananchi nchini humo. Hivi karibuni pia akiwa katika kikao cha baraza la mawaziri wa nchi hiyo, Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi akiyaonya makundi ya kisiasa juu ya njama za kuibua tofauti na kuvitaka vyama na makundi ya kisiasa nchini humo kufanya juhudi za kuhimiza umoja na mshikamano dhidi ya njama hizo za uhalifu ambazo zinawakabili Wairaq wote. Al-Abadi alivitaka vyombo vya habari kuimarisha umoja wa kitaifa na utulivu wa ndani ya nchi na kwamba wote kwa pamoja wanatakiwa kukabiliana na waharibifu wa mali za umma bila kujali tofauti.
Akizungumzia njama za kuibua fitina za kikaumu na kimadhehebu nchini, Waziri Mkuu wa Iraq alisema kuwa, kufuatia kushindwa mtawalia magaidi wa kitakfiri wameelekeza nguvu zao kwenye suala la kuzusha fitina za kikaumu nchini humo na kwamba Wairaq wote wanatakiwa kuwa macho mbele ya njama hizo.

Tuesday, 19 January 2016
Leo ni Jumanne tarehe 8 Rabiuthani 1437 Hijria sawa na 19 Januari 2016.
Siku kama ya leo miaka 1205 iliyopita alizaliwa Imam Hassan Askari (as) ambaye ni miongoni mwa wajukuu wa Mtume Muhammad (saw) katika mji mtakatifu wa Madina. Imam Askari alilazimishwa na watawala wa Bani Abbas kwenda uhamishoni huko Samurra akiwa pamoja na baba yake na kufaidika na elimu ya Imam Hadi kwa kipindi cha miaka 13. Alishika hatamu za kuongoza Umma wa Kiislamu kwa kipindi cha karibu miaka sita baada ya kuuawa shahidi baba yake. Sehemu ya umri wake wa miaka 28 uliishia katika jela za watawala madhalimu wa Bani Abbas au akiwa uhamishoni na chini ya udhibiti wa watawala hao. Hata hivyo mtukufu huyo hakuacha kueneza maarifa sahihi ya Uislamu na kulea kizazi cha wanazuoni hodari.
Siku kama hii ya leo miaka 280 iliyopita alizaliwa mvumbuzi na mhandisi wa Kiingereza James Watt. Msomi huyo alipendelea na kuvutiwa mno na utafiti kuhusu masuala ya kisayansi. Katika utafiti wake Watt alifanikiwa kuvumbua nishati ya mvuke na kuzusha mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda hususan usafirishaji wa nchi kavu na baharini.
Siku kama ya leo miaka 37 iliyopita, wananchi Waislamu wa Iran wenye imani na umoja walifanya maandamano makubwa kupinga mabaki yaliyosalia ya utawala wa kifalme Shah, yaani serikali ya Shapur Bakhtiyar. Wafanya maandamano hao walitaka serikali hiyo ya kifalme itangazwe kuwa si halali, na pia kung'olewa utawala wa Shah na badala yale kuundwa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran. Siku hiyo Imam Khomeini MA akiwa mjini Paris alitoa ujumbe wa maandishi kwa wananchi wa Iran akisema kama tunavyonukuu: "Kwa uwezo wake Mola hivi karibuni nitaungana nanyi ili niweze kuwatumikia na kushirikiana bega kwa bega na matabaka yote ya wananchi kuelekea katika njia ya kujitawala na kuwa huru Iran." Mwisho wa kunukuu.
Katika siku kama ya leo miaka 6 iliyopita, Abdul Rauf Mahmoud al-Mabhuh, mmoja wa makamanda waandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS aliuawa shahidi huko Dubai, katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Mabhouh aliuawa na makachero wa Shirika la Ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel walioingia nchini Imarati wakitumia pasipoti bandia. Mabhuh alizaliwa katika familia iliyoshikamana na dini katika kambi ya Jabalia katika Ukanda wa Gaza, Palestina. Shahidi Mahmoud al-Mabhuh ni miongoni mwa waasisi wa Brigedi ya Izzudeen al-Qassam tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Baada ya kupita miezi kadhaa, Israel ilitangaza wazi kwamba, ilihusika na jinai ya kumuua Mabhuh.
Jumanne, 19 Januari 2016 10:51
Zarif: Saudia inaeneza chuki dhidi ya Iran M/Kati

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, utawala wa Aal-Saud wa Saudi Arabia unaeneza chuki na propaganda dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ili kuibuka taharuki katika eneo la Mashariki sambamba na kufanikisha ajenda zake.
Katika mahojiano na kanali moja ya televisheni hapa nchini, Muhammed Javad Zarif amesema, wasi wasi wote huo wa serikali ya Riyadh umetokana na kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya nyukia ya Iran.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema miongoni mwa mbinu zinazotumiwa na utawala wa kifalme wa Saudia ili kuzusha hofu katika eneo ni hatua yao ya hivi karibuni kushusha bei ya mafuta na kusisitiza kuwa: “Kupunguza bei ya mafuta ina taathira hasi kwao, kulikoni kwetu.
Muhammed Javad Zarif ameongeza kuwa, Saudia haiwezi kufanikisha sera zake kwa kueneza chuki na propaganda dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa Jumamosi iliyopita na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya huko mjini Vienna, Austria, vikwazo vyote vya kifedha, uchumi na vinginevyo vinavyohusiana na mpango wa nyuklia wa Iran vimeondolewa rasmi kuanzia tarehe 16, Januari mwaka huu, kwa mujibu wa makubaliano hayo ya nyuklia yanayojulikana kama JCPOA.
Tuesday, 12 January 2016
Assalamu Alaykum warahmatullahi taala Wabarakatuhu.leo tujifunze somo la kwanini yawepo maradhi.mwenyezmungu anasema katika kitabu chake kitukufu. "na kwa Hakika tutawajaribu kwa jambo la khofu na njaa na upungufu wa wa mali na nafsi na matunda, nawe wape habari ya furaha wenye kusubiri. Ambao ukiwafika msiba, husema :Hakika sisi ni wa mwenyezimungu na sisi tu wenye kurejea kwake. Hao juu yao ziko baraka na rehema kutoka kwa mola wao, nao ndio wenye kuongoka (baqara:155-157)aya hiyo inaeleza suala la majaribu ya mwenyezimungu kwa waja wake katika nyanja mbali mbali, kwa mujibu wa Aya hiyo tukufu tunaelezwa kuwa nusura hapatikani kwa njia yeyote ispokuwa chini ya kivuli cha subira na kutawakali kwa mwenyezimungu.kwahiyo yanakuwepo maradhi kwa ajiri ya mwenyezimungu kuwajaribu waja wake . inshaallah tutaendelea.
Shein: Wazazibari jiandaeni kwa uchaguzi wa marudio

Katika kile kinachoonekana ni kuvurugika mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar, pande husika katika mazungumzo hayo zimetoa misimamo inayokinzana kikamilifu.
Sira ya Imam Sadiq (AS) ya Waislamu kuridhiana na kuwa wamoja

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Siku ya Ijumaa ya mwezi 17 Mfunguo Sita (Rabiul-Awwal) mwaka 83 Hijria, sawa na mwaka 702 Miladia, alizaliwa mja mbarikiwa, Imam Jaafar As-Sadiq (AS); shakhsia mkubwa katika Ahlul Bayt wa Bwana Mtume Muhammad SAW, ambaye jina lake limezipamba duru za kielimu na kidini katika zama zote za historia. Katika siku hii ya leo yenye baraka, inayosadifiana pia na maadhimisho ya maulidi ya Mtume wa mwisho wa Allah, Nabii Muhammad SAW, tunamswalia na kumtakia rehma na amani mtukufu huyo na mbora huyo wa viumbe pamoja na Ahlul Bayt zake sambamba na kukupeni nyinyi wapenzi wasikilizaji mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba huo.
Karibuni basi kusikiliza kipindi hiki maalumu kitakachodondoa machache katika sira ya Imam Sadiq (AS) kuhusu umoja baina ya Waislamu.
Imam Jaafar As-Sadiq (AS) alitumia kipindi cha miaka 34 ya umri wake wa miaka 65 kubeba mas-ulia mazito na hasasi ya Uimamu na uongozi wa umma wa Kiislamu. Kati ya Ahlu Bayt wa Bwana Mtume SAW, hakuna yeyote miongoni mwao aliyepata fursa kubwa zaidi kama aliyopata yeye ya kueneza mafundisho ya Uislamu na kuandaa shakhsia wateule na watajika. Zama za Imam Sadiq (AS) zinaweza kutajwa kuwa ni zama za migongano ya fikra na kuibuka madhehebu na matapo mbalimbali. Jambo hili lingeweza kuikosesha jamii ya Kiislamu mafundisho halisi ya dini hiyo na kuwaelekeza watu kwenye upotofu; lakini kuwepo kwa nuru ya shakhsia ya Imam Jaafar As- Sadiq (AS) kuling'arisha anga ya fikra za wenye kiu ya haki na kuwaacha vinywa wazi watu waliokuwa wakijigamba kuwa wajuzi wa elimu na maarifa.
Imam Sadiq (AS) alikuwa akisistiza kila mara juu ya kuwepo uhusiano wa kiutu na wa upendo mkubwa baina ya watu. Alikuwa akisema: "Shikamaneni, pendaneni, tendeaneni wema na ihsani na oneaneni huruma". Mtukufu huyo alikuwa akiusia mtu kuwa na upendo na urafiki na Waislamu wote; na hata akamuusia mmoja wa masahaba zake kwa kumwambia:" Wafikishie salamu wafuasi wetu na waambie Mwenyezi Mungu anamrehemu mja anayejijengea urafiki kwa watu".
Imam Jaafar As-Sadiq (AS) alikuwa akiamini kwamba watu wa jamii tofauti za kidini ni sehemu ya Jamii ya Kiislamu na wanapaswa kuheshimiwa. Yeye mwenyewe alikuwa katika zama ambazo waliishi ndani yake watu wa dini na madhehebu mbalimbali. Tunapoutalii mwamala na mlahaka wa Imam Sadiq kwa wafuasi wa dini na madhehebu nyengine tutabaini kwamba mtukufu huyo alikuwa akiwapokea katika darsa zake Waislamu wa madhehebu mbalimbali bali hata na wasiokuwa Waislamu. Abu Hanifa, Imam wa madhehebu ya Hanafi ni miongoni mwa watu hao, ambapo yeye mwenyewe aliwahi kusema, lau isingelikuwa miaka miwili aliyosoma kwenye darsa ya Imam Sadiq (AS), basi angeangamia.
Mlahaka huo wa Imam Jaafar As-Sadiq (AS) ulileta faida nyingi sana kwa jamii ya Waislamu wa zama hizo. Miongoni mwa hizo ilikuwa ni ya watu kukutanika pamoja na kujdiliana, ambapo hata kama majadiliano yao hayakuishia kwa mmoja kukubali fikra na rai ya mwenzake, lakini yalijenga upendo na kuwafanya wamoja. Kwa sababu wakati watu wanapokaliana mbali hufikiriana dhana mbaya, na hilo ni jambo linalochangia sana kuwepo suutafahamu baina yao. Kuonana uso kwa uso kuna taathira kubwa ya kumfanya mtu awe na ufahamu sahihi na wa pande zote wa itikadi na mitazamo ya wenzake. Kuhudhuria darsa za Imam Sadiq (AS) kuliwafanya watu wenye fikra nyenginezo wamfahamu vizuri na kwa karibu zaidi Imam na kutambua adhama yake ya kielimu na utukufu wake wa kiroho. Kwa hakika sira hiyo ya tadbiri na hekima ya Imam Jaafar As-Sadiq (AS) inapasa kuwa dira na mwongozo wa kufuatwa na madhehebu mbalimbali; kwani sababu kubwa inayozifanya madhehebu leo hii ziwe mbalimbali ni suutafahamu juu ya itikadi na matendo baina ya madhehebu moja na nyengine. Na ni suutafahamu hiyo, ndiyo inayotumiwa na maadui kusababisha na kuchochea chuki na uadui baina ya Waislamu wenyewe.
Japokuwa watu waliokuwa wakishiriki kwenye darsa za Imam Jaafar As-Sadiq (AS) hawakuwa na mtazamo sawa kifikra na mtukufu huyo lakini walikuwa wakiitukuza daraja yake ya elimu na kukiri kwamba hawakuwahi kuona faqihi mkubwa zaidi ya Imam. Tab'an kuna idadi kubwa ya wanafunzi na wahudhuriaji wa darsa za Imam Jaafar As-Sadiq waliofuata njia yake. Mfano mmoja maarufu wa wanafunzi hao ni Hisham Ibn Hakam. Vitabu vya hadithi na historia vya Shia na Suni vimesimulia mengi kuhusu midahalo na mijadala aliyofanya Imam Jaafar As-Sadiq (AS) na viongozi wa madhehebu, wa kidini na hata wasio wa kidini wa zama zake. Lakini nukta muhimu ni kwamba mijadala hiyo haikuishia kwenye utengano wala uhasama. Kwani moja ya usuli ya kiakhlaqi ya Imam ilikuwa ni kushikamana na wasia wa Qur'ani usemao "jaadilhum billatii hiya ahsan", yaani kujadiliana na watu kwa upole na kwa wema. Kwa hivyo hata wapinzani wenyewe walikuwa wanakiri kwamba Imam Jaafar Sadiq alikuwa akichunga heshima ya mtu anayejadiliana naye na kusikiliza maneno yake hadi mwisho kwa hamu, utulivu na umakini. Kisha kwa kutumia maneno sahihi na yaliyokamilika, lakini machache na yenye kufikisha ujumbe, ndipo na yeye akawa anabainisha rai na maoni yake.
Kuhusu ulazima wa kudumisha umoja na kuwa kitu kimoja, Imam Sadiq (AS) alimueleza mmoja wa masahaba zake alitwaye Zaid Ibn Hisham kuhusu jinsi ya kulahikiana na kuamiliana na wafuasi wa madhehebu nyengine za Kiislamu kwa kusema:
"Ingieni na salini misikitini mwao; watembeleeni wagonjwa wao; shirikini kwenye maziko yao; na kuweni na tabia ya namna itakayowafanya wakujieni na kusali nyuma yenu....Mwenendo wenu utakapokuwa huo watasema, hawa wana madhehebu ya Jaafarii; Mwenyezi Mungu amrehemu Imam Sadiq, amelea wafuasi wazuri walioje.... Lakini kama akhlaqi zenu zitakuwa mbaya;... watasema hawa ni wafuasi wa Jaafari, na Imam Sadiq amelea wafuasi wabaya walioje."
Katika mahala pengine Imam Jaafar Sadiq (AS) amesema: "Muislamu ni ndugu wa Muislamu, na ni sawa na jicho, kioo na muongozo kwake; katu hamsaliti; hamhadai; hamdhulumu; hamwambii uongo na wala hamsengenyi."
Kwa hivyo kwa mtazamo wa Imam Jaafar Sadiq (AS) misingi ya kuimarisha na kuiunganisha jamii ya Waislamu ni kuwa na nia njema, kutakiana kheri, kushirikiana na kusaidiana. Ni matarajio hewa kudhani kwamba tutaweza kuwa na umma imara na ulioshikamana pasina kuandaa misingi hiyo ya kimwenendo na kitabia. Tuelewe kwamba mifarakano na kudhoofika kwa jamii ya Waislamu chimbuko lake ni utengano uliopo baina ya nyoyo za Waislamu wenyewe na kushamiri umimi na ubinafsi kati yao.
Wapenzi wasikilizaji, kwa mara nyengine tena ninachukua fursa hii kukupeni mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba wa siku hii ya kuadhimisha kuzaliwa Imam Jaafar As-Sadiq (AS). Ni matumaini yangu kuwa sira na miongozo ya mtukufu huyo itakuwa taa ya kumurikia na kuongozea njia kwa Umma wa Kiislamu kwa ajili ya kuleta umoja na mshikamano baina ya Waislamu duniani. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Nasrallah: Kunyongwa Sheikh Nimr ni jinai ya kutisha

Katibu Mkuu Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameitaja kuwa jinai ya kuogofya hatua ya utawala wa Saudia Arabia kumuua shahidi mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Saudia Sheikh Nimr Baqir al Nimr.
Sayyed Hassan Nasrallah ameyasema hayo Jumapili mjini Beirut katika hotuba ya moja kwa moja kwa njia ya Televisheni Jumapili katika hafla ya kumkumbuka marhum Sheikh Mohammad Ali Khatoun, mwanachama mwandamizi wa harakati hiyo. Akiashiria jinai ya Saudi Arabia katika kumnyonga Sheikh Nimr, amesema haiwezekani kufumbia macho jinai hiyo ya kinyama dhidi ya mwanazuoni huyo wa ngazi za juu.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria umuhimu na hadhi aliyokuwanayo Sheikh Nimr kwa umma wa Kiislamu na kusema kuwa, utawala wa Aal Saudi unadai kutetea demokrasia na uhuru katika eneo lakini unapinga kukosolewa huku ukiwakandamiza wale wanaotaka mabadiliko.
Sayyid Hassan Nasrallah amesema Sheikh Nimr daima alifuata mkondo wa amani kama maulamaa wengine wa mashariki mwa Saudia na Bahrain. Ameongeza kuwa vyombo vya mahakama vya Saudia vimemyonga Sheikh Nimr kutokana na ushujaa wa aina yake aliokuwa nao mwanazuoni huyo mkubwa na mwanamapambano. Amesema mahakama za utawala wa Saudia hazikuweza kuthibitisha madai yao dhidi ya mwanazuoni huyo.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa mahakama za Saudia zilitoa madai yasiyo na msingi dhidi ya Sheikh Nimr kuwa eti alikuwa na silaha na kwamba eti aliunda kundi lenye silaha kukabiliana utawala wa kifalme nchini humo na kusema kuwa, wakuu wa Saudia walihisi kuwa ushujaa na kauli ya haki ya mwanazuoni huyo ni tishio kwao.
Sayyid Nasrallah ameendelea kusema kuwa, kwa kuuawa shahidi na kidhulma, Sheikh Nimr amefuata mkondo na mitume na chuo cha Karbala. Kiongozi wa Hizbullah ametuma salamu zake za rambi rambi kwa familia ya Shahidi Sheikh Nimr, Waislamu na maulamaa wa Kiislamu kote duniani. Huku akilaani vikali jinai hiyo ya Saudia ya kumuua Sheikh Nimr, Sayyid Nasrallah amesema Saudi Arabia itafeli katika njama zake za kuvuruga harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon.
Subscribe to:
Posts (Atom)